Afisa utumishi wa Halmashauri Tarime mjini afutwa kazi


Halmashauri ya Tarime mji imemsimamisha kazi na kisha kuamuru kukamatawa na kufikishwa mahakamani afisa utumishi mwandamizi wa halmashauri hiyo Bw. MWITA RAULENT kwa tuhuma ya ubadhilifu wa fedha zaidi ya shilingi milion 28 huku tuhuma hizo zikiwahusisha watumishi wengine wapatao sitini kutoka halmashauri hiyo ambao wamepewa siku tatu za kujieleza na endapo nao watabainika kuhusika moja kwa moja na ubadhilifu huo watapewa adhabu kali kwa mujibu wa sheria.

Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa Halmashauri ya Tarime mji Bw. ELIAS NTIRUHUNGWA alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mara baada ya kumaliza mkutano wake watumishi wa Halmshauri hiyo.

Amesema kitendo kilichofanywa na afisa huyo kutumia wadhifa alionao akishirikiana na baadhi ya watumishi wa halmshauri hiyo kukwepa kulipa mikopo kutoka taasisi za fedha ni aibu kubwa kwa halmshauri hiyo na hivyo ni lazima sheria ifuate mkondo wake ili iwe fundisho kwa watumishi wengine wenye tabia kama hizo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo