Madereva na watumiaji
wa mabasi katika stendi ya mkoa wa Njombe wameiomba halmashauri ya mji huo
kukarabati barabara zinazoelekea vijijini kutokana na kuharibika baada ya mvua
kubwa kunyesha
Wakizungumza na
mwandishi wetu madereva hao wamedai kuwa barabara nyingi zinazoelekea vijijini
zimeharibika kitendo kinachopelekea kuchelewa kufika safari zao na hivyo
kuonekana ni usumbufu kwa wateja wao ambao ni abiria
Nao baadhi ya abiria
wamesema ubovu wa barabara hizo huwalazimu muda mwingine kushuka katika magari
na kutembea kwa miguu
Ibrahimu Mkangala ni
Mhandisi wa halmashauri ya mji wa Njombe ambaye amewataka watumiaji wa vyombo
vya usafiri kuwa wavumilivu kwani halmashauri hiyo tayari imeshapanga mikakati
ya kukarabati barabara hizo zilizoharibika mara tu mvua zitakapokwisha
Katika hatua nyingine
mhandisi huyo ametolea ufafanuzi ukarabati wa stendi hiyo ya muda ya mabasi
mkoani Njombe