Waheshimiwa Madiwani wa jiji la Dar es Salaam
Ndugu Wananchi wa jiji la Dar es Salaam
Waandishi wa habari
Heri ya siku kuu ya Pasaka.
Ndugu wananchi wa Jiji la Dar es Salaam.
Napenda kutumia nafasi hii kwanza kabisa kumshukuru mwenyezi mungu kwa kuniwezesha kuwa mzima hadi siku hii ya leo. Ni dhahiri kwamba mmekuwa pamoja tangu nilipochaguliwa kuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam. Lakini pia mmekuwa bega kwa bega na mimi Meya wenu wa Jiji, katika juhudi kubwa za kulifanya jiji letu kuwa la kuvutia. Hivyo nina kila sababu ya kuwashukuru na kuwapongeza sana.
Ushirikiano ambao mnaunyesha na kuendelea kuuonyesha unanipa matumani makubwa kwamba tuko pamoja katika kuhakikisha kwamba tunaleta mabadiliko makubwa katika jiji letu na hivyo kuondokana na changamoto mbalimbali zinazo likabili jiji letu. hivyo naomba tuendelee kushirikiana na kuzidi kuniombea Meya wenu niweze kufanya kazi ambazo mmenituma katika jiji letu la Dar es Salaam.
Ni wazi mnafahamu kwamba, maendeleo ya jiji letu hajawezi kuletwa bila ya nyinyi wannachi kuonyesha ushirikiano kwa viongozi wenu ambao mmetuchagua kuanzia ngazi za Mitaa, Kata, Halmashauri pamoja na jiji.
Ndugu wananchi wa Jiji la Dar es Salaam.
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imekuwa na mipango mingi mizuri ambayo imelenga kuboresha maendeleo ya wananchi wake. Miongoni mwa mambo ambayo niweka na kuendelea kusimamia ili kuhakikisha kwamba wakazi wa jiji la Dar es Salaam wanapata huduma mbalimbali za kijamii kwa uhakika.
Ndugu wananch wa Jiji la Dar es Salaam.
Hivi sasa tunaingia kwenye kipindi cha sikuu ya pasaka. Tunapoungana na wenzetu Wakristo katika kusherehekea Sikukuu ya Pasaka, niwaombe wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuendeleza kushirikiana na vyombo vyetu vya usalama katika suala zima la uimarisha wa usalama wenu.
Vyombo vya usalama vimekuwa rafiki kwa kipindi chote jambo ambalo limefanya kupungua kwa matukio ya kiuhalifu ndani ya jiji letu.
Hivyo basi nitoe rai kwa wakazi wote wa jiji la Dar es Salaam, kusherehekea siku kuu hii kwa Amani na utulivu bila kuwepo kwa vurugu zozote. Salamu zangu za upendo katika sikukuu hii ya Pasaka ziwe chachu ya kuendelea kutunza amani katika jiji letu, huku mki hakikisha kwamba kila eneo ambalo watoto wenu watashiriki kwa namna moja ama nyingine kuwe na usalama wa uhakika. Tusijenge utamaduni wakukubali matukio ya kuvunja amani kwenye siku kuu maana hizi ni sherehe sio vita.
Ndugu wananchi wa Jiji la Dar es Salaam,
Mtakubaliana name kwamba, Siku kuu hii imekuja na neema ya mvua, ukizingatia ni jambo ambalo tulikuwa tukililia kwa muda mrefu sana ili kuondokana na hali ya ukame. Napenda kutumia fursa hii kuwataka wale wote ambao wapo maeneo ya hatarishi (mabondeni), kuanza kuchukua tahadhari mapema kabla ya kukumbwa na adha ya mafuriko.
Sote ni mashahidi kwamba, wakati wa mvua kama hizi kumekuwa na madhara makubwa ambayo hujitokeza kwa wale ambao huishi mabondeni. Hivyo kama jiji linampango mkakati wa kuboresha miundombinu ya maji ili kuepukana na adha hii ya mafuriko. lakini basi wakati jiji likiwa kwenye mkakati huo, tuchukue tahadhari mapema kabla ya kuleta maafa.
Ndugu wananchi wa jiji la Dar es Salaa.
Nimekuwa katika majukumu mbalimbali ya kitaifa kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wetu. Nitoe rai kwa wananchi kushirikiana na viongozi mliowachagua ili kuweza kuwasilisha kero zenu sehemu husika ili mamlaka ziweze kushughulikia kero hizo mapema.
Aidha Ofisi ya Meya wa jiji imekuwa rafiki kwa wananchi wote katika kuhakikisha kwamba tunakuwa na Jiji ambalo linajali mahitaji mbalimbali ya wananchi wake hususani wafanyabiashara wadogowadogo, Bodaboda, Mama lishe, na makundi mengine mbalimbali.
Ndugu wananchi wa Jiji la Dar es Salaam.
Halikadhalika pia, napenda kuvipongeza vyombo vyote vya habari kwa mchango mkubwa ambao mnaonyesha wa kuhabarisha Umma wa wa Tanzania mambo mbalimbali yanayofanywa na jiji. na kwamba mmekuwa ni chachu kubwa ya kutangaza shughuli mbalimbali zinazofanywa na jiji. Niseme tu kwamba jiji la Dar es Salaam, linatambua mchango wenu mkubwa na kuwaomba muendelee kufanya kazi zenu kwa weledi mzuri na kwamba tuko pamoja na nyie.
Ndugu wananchi wa Jiji la Dar es Salaam.
Mwisho kabisa niwatakie maandalizi mema ya sikukuu ya Pasaka ,iwe na heri na fanaka kwa watu wote, na kwamba mapumziko haya ya siku tatu, muyatumie kwa kulijenga jiji lenu badala ya kulibomoa.
Mwisho kabisa napenda kuwatakia sikukuu njema
Mungu ibariki Tanzania , mungu libariki jiji la Dar es Salaam.
Imetolewa na Mstahiki Meya wa jiji
…………………….
Isaya Mwita Charles.