Vurugu imetokea leo wakati kundi la watu wanaodaiwa kuwa wanachama wa chama kimoja cha siasa (jina kapuni hadi itapothibitishwa) kupambana na wenzao wanaosadikiwa kuwa wapinzani wao baada ya kundi moja kuvamia mkutano wa upande mmoja na waandishi wa habari katika Hotel ya Vinna Hotel maeneo ya Mabibo jijini Dar es salaam, na kuzua taharuki kubwa kwa waandishi wa habari na wakaazi wa eneo hilo.
Mashuhuda wamesema watu kadhaa wasiojulikana walifika hapo wakiwa wamefunika nyuso zao kwa vitambaa huku wakiwa na silaha za jadi na kuanza vurugu.
Baada ya mkutano kuvurugika baadhi ya waliokuja kufanya vurugu walikimbia huku wakikimbizwa na wanachi wenye hasira kali ambao walifanikiwa kumkamata mmoja wao na kumjeruhi kwa kumkata maungio ya kisigino ya mguu wake wa kulia.
Juhudi za kuwapata wasemaji wa pande mbili hizo zinaendelea