Mama mzazi adai kuibiwa mtoto mmoja baada ya Kujifungua Mapacha Temeke

Tukio lilionekana kuwa ni la utata limetokea katika Hospitali ya rufaa ya Temeke ambapo Mwanamke mmoja alietambulika kwa jina la  Asma Juma kudai kuibiwa mtoto wake baada ya kujifungua mapacha na kukabidhiwa mtoto mmoja kati ya wawili hao.
Wakazi wa Kata ya Chamazi mtaa wa Pande, Asma Juma na Mumewe, Abubakar Pazi wakimfurahia mmoja wa mtoto wao wanayedai alizaliwa mapacha katika Hospitali ya Rufaa ya Temeke Dar es Salaam, mwezi uliyopita na mmoja kupotea katika mazingira yasiyofahamika. Picha na Salim Shao
Asma alisema kabla ya kupewa rufaa ya kwenda kujifungua katika hospitali hiyo, alipima kipimo cha ‘ultrasound’ na kuthibitishiwa kuwa ana mapacha.
Asma alisema awali alikuwa akipata huduma za kliniki katika Zahanati ya Serikali ya Mbande, lakini alikuwa amefanya vipimo vya ‘Ultrasound’ katika Zahanati ya binafsi ya Huruma iliyopo Mbande mara mbili na kuthibitishiwa kuwa ana pacha.
“Wakati napelekwa chumba cha upasuaji nilikuwa sina kichaa cha uzazi, siumwi uchungu, siumwi kichwa, siyo kipofu, siyo kiziwi, nasikia kwa masikio yangu na kumbukumbu zote nimezihifadhi kwenye kichwa changu. Ninachotaka ni mtoto wangu,” alisema Asma.
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke, Dk Gwamaka Mwabulambo alikiri kuwapo kwa tuhuma hizo na kusema tayari zinafanyiwa kazi na uongozi.
Chanzo: Mwananchi


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo