AUDIO: Maajabu mengine ya jiji la Dar, mwanamke adaiwa kufa kisha kufufuka

Asubuhi ya April 18, 2017 kulisambaa taarifa za kufufuka kwa mwanamke ambaye alidaiwa kufa baada ya kugongwa na gari usiku wa kuamkia leo na kuthibitishwa kifo chake.
Mwanamke huyo anayefahamika kwa jina la Anna mkazi wa Tanki Bovu jijini Dar es Salaam anadaiwa kugongwa na gari usiku wa April 17, 2017 siku ya Pasaka kisha kufanyiwa vipimo na kuthibitika kuwa kweli amefariki, lakini taarifa za kifo hicho ziliposambaa ndipo zikaibuka taarifa nyingine kuwa angali hai.
Katika hali ya kustaajabisha, vijana wawili waishio mtaa mmoja na mwanamke huyo walijitokeza na kudai kuwa mwanamke huyo hakufa bali yupo hai amechukuliwa kimazingara.
Chanzo:millardayo
Bonyeza play kusikiliza ilivyokuwa:-


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo