Katibu Mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad amesema bado anajitambua kuwa yeye ndiye katibu Mkuu wa Chama hicho na Maamuzi ya Prof Lipumba kutangaza kuwa Naibu Katibu Mkuu bara Magdalena Sakaya kukaimu nafasi yake ni batili
Maalim Seif ameyasema hayo wakati akihojiwa na kituo cha Televisheni cha Azam, ambapo amesema pamoja na yote hatafika kwenye ofisi za CUF Buguruni kwa kuwa sio makao Makuu ya Chama hicho bali ni ofisi kuu tu
Amesema anaendelea na ziara za chama hicho katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar,na akimaliza ataanza Ziara jijini Dar Es Salaam
Unaweza kumsikiliza Maalim Seif kwa kubonyeza Play hapo chini:-
