ATCL imetoa matokeo ya ndege zake baada ya muda wa Miezi 4

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la (ATCL), Lasislaus Matindi amesema wamefanikiwa kukusanya shilingi Bilioni 9 kwa miezi minne tu kwa kutumia ndege mbili zilizonunuliwa na Serikali ya Rais Dkt John Pombe Magufuli.

Ndege hizo zilianza kufanya kazi Oktoba 2016 baada ya kuzinduliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli mwezi Septemba  2016 ambapo zilinunuliwa kwa fedha taslimu kutoka Kampuni ya nchini Canada.
Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) ilianzishwa mwezi Novemba 2002 baada ya Serikali kubinafsisha lililokuwa Shirika la Ndege la Tanzania (Air Tanzania Corporation, ATC). Katika Shirika hilo, Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) lilinunua hisa asilimia 49 ndani ya ATC. Hata hivyo ubia kati ya ATCL na SAA ulikabiliwa na matatizo ya kiuendeshaji na kulazimika kusitishwa mwezi Agosti 2006 na ATCL kurejeshwa tena Serikalini kwa asilimia 100.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la ATCL, Bw. Lasislaus Matindi anasema wamefanikiwa kukusanya Shilingi Bilioni 9 kwa Miezi minne tu kwa kutumia ndege hizo mbili zilizonunuliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, nakuleta utata mkubwa na wapinzani wa siasa nchini waliodai kuwa hazikuwa na tija kwa Taifa.

Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) ilianzishwa mwezi Novemba 2002 baada ya Serikali kubinafsisha lililokuwa Shirika la Ndege la Tanzania (Air Tanzania Corporation, ATC); katika Shirika hilo, Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) lilinunua hisa asilimia 49 ndani ya ATC. Hata hivyo ubia kati ya ATCL na SAA ulikabiliwa na matatizo ya kiuendeshaji na kulazimika kusitishwa mwezi Agosti 2006 na ATCL kurejeshwa tena Serikalini kwa asilimia 100.
KUMBUKUMBU:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na maafisa na viongozi wengine mbalimbali akikata utepe kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam Jumatano Septemba 28, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na maafisa wengine waandamizi wakiwa kwenye ndege mojawapo baada kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam Jumatano Septemba 28, 2016. PICHA NA IKULU.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo