JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TUME YA MABADILIKO YA KATIBA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TUME YA MABADILIKO YA KATIBA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Hafla ya kukabidhi Rasimu ya Katiba kwa Mhe. Rais
Tume ya Mabadiliko ya Katiba inapenda kuwafahamisha wananchi na wadau wengine wote kuwa Hafla ya kukabidhi Rasimu ya Katiba kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mhe. Dkt. Ali Mohammed
Shein, Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi itafanyika siku ya
Jumatatu, Desemba 30, 2013 katika Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es
Salaam.
Hafla hiyo pia inatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, taasisi za kidini, asasi za kiraia na wananchi wa kawaida.
Taarifa zaidi kuhusu hafla hii zitatolewa baadaye.
Imetolewa na:
Imetolewa na:
Assaa Rashid,
Katibu,
Tume ya Mabadiliko ya Katiba,
Dar es Salaam
Desemba 19, 2013.