Rungu Jingine, Wamiliki na Wauzaji wa "Chain Saw" Mjiandae

Serikali inakusudia kuandaa mwongozo wenye lengo la kusajili wamiliki na wauzaji wote wa misumeno ya umeme maarufu kama "chain saw" ambayo inatumika kukatia miti na magogo porini.
Mwongozo huo wa serikali unalenga kudhibiti uvunaji wa misitu unaofanywa na watu wasio na vibali, ambao wamekuwa wakinunua holela madukan misumeno ya umeme na kuingia misituni kukata miti kwa kiwango kikubwa.
Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais Muungano na mazingira January Makamba amesema utaratibu huo mpya unakusudia kuzuia uuzaji holela pamoja na kuwataka wanaotumia kuwa na vibali rasmi vya serikali vya uvunaji wa miti.
Akizungumza na watendaji wa wilaya ya korogwe mkoani Tanga na same mkoani Kilimanjaro, waziri Makamba amezitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha zinakuwa na orodha ya shughuli zinazostahili kuwa na vyeti vya tathmini ya athari za mazingira na wasio kuwa navyo watozwe faini.
Ametaka ukaguzi ufanyike kwa kila halmashauri kwa kushirikiana na maafisa kutoka baraza la taifa la usimamizi wa mazingira NEMC ili Kukamilisha ukaguzi huo.
Akiwa wilayani same, mkuu wa wilaya hiyo Rosemary Senyamule ameiomba serikali kuu kuwasaidia namna ya kudhibiti maporomoko ya maji ya mvua yanayotoka milimani ambayo yamekuwa yakiharibu mazingira kwa kusababisha mmomonyoko wa ardhi na makorongo makubwa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo