Mwanafunzi Yuko Hoi Hopsitalini Njombe baada ya Mwalimu Kumchapa Viboko 10

Mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi madeke halmashauri ya wilaya ya Njombe mwenye umri wa miaka 10 inadaiwa kuwa anaendelea kuugulia maumivu ya adhabu ya kuchapwa viboko visivyopungua 10 na mwalimu wake wa hesabu baada ya kufeli somo hilo hapo Machi 21 mwaka huu

Kwa mujibu wa baba  mzazi wa mtoto huyo Bonface Manga Kwa masharti ya kutorekodiwa na waandishi  mwanae Hosea Manga alichapwa viboko kumi na mwalimu wake na kisha akazidiwa na kukimbizwa hospitali.

Kutoka hospitali ya teule ya Mkoa wa Njombe Kibena ambako mtoto  huyo amelazwa hali yake bado ingali si nzuri kwa kuwa hawezi kusimama wala kutembea licha ya kaimu mganga mfawidhi Wa hospitali hiyo Isaya Mvinge kueleza kuwa uchunguzi wa kitabibu bado unaendelea

Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Njombe Kupitia Mkurugenzi Mtendaji Monica Kwiluvya anakiri kupokea taarifa kwa njia ya simu kutoka kwa afisa elimu kata kuwa mwalimu aliyehusika anashikiliwa na polisi

Jitihada za kupata taarifa ya jeshi la polisi zimegonga mwamba baada a kamanda wa jeshi la polisi kueleza kuwa yuko nje ya mkoa kikazi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo