Mwalimu Jela miaka 4 kwa kumkashifu mwanafunzi wake

Mahakama ya Wilaya mwanakwerekwe imempeleka chuo cha mafunzo miaka 4 khamis Zahir mwalim (24) mkaazi wa  Mfenesi maziziz Wilaya ya Mjini kwa kosa la kumkashifu mwanafunzi wake.
Imeadaiwa Mahakamni hapo na muendesha mashtaka wa Serikali Saidi Ali na Huda Othaman mbele ya hakimu Chausiku  Kafuti Mkuya kwamba siku ya tarehe 17 disemba 2015 majira ya saa 3 asubuhi huko gulioni mshtakiwa ambe ni mwalimu wa Almadrasat  Nnabiy iliyoko Gulioni alimshika na kunyonya matiti mwanafunzi wake wa kike mwenye umri wa miaka 13 jambo ambalo ni kosa kisheria
Awali aliposomewa kosa lake mshtakiwa alikataa nakupandishwa kizimbani kwa nyakati  tofauti na Jana kusomewa hukumu yake.
Mshtakiwa amepelekwa chuo cha mafunzo miaka 4 ili akajifunze tabia njema na iwe funzo kwake na wengine wenye tabia kama hiyo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo