Makonda abanwa Dodoma, Wanafunzi wamtaka aoneshe Vyeti Vyake

Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa mkoani Dodoma alizua gumzo baada ya kuulizwa swali na mwanafunzi mmoja kuhusu tuhuma za vyeti vyake zinazomkabili ambapo kwa siku zote amekuwa yupo kimya kuhusu tuhuma hizo.
Mwanafunzi huyo alimuomba RC Makonda kulitolea ufafanuzi tuhuma za vyeti inayomkaili kama suala hilo lipo ndani ya uwezo wake kwani ni kiu ya watu wengi kutaka kuufahamu ukweli wote sababu pamekuwepo mengi yaliyosemwa.
RC Makonda alipoanza kujibu swali hilo alisema kuwa suala hilo halihitaji hata mtu awe amekwenda shule badala yake ukitumia tu akili ya kuzaliwa utaweza kupata jibu. Amesema kuwa yeye tangu ameanza kupigania haki za wanyonge kila siku zimekuwa zikiibuliwa kashfa mpya kuhusu yeye.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo