NA SALVATORY KUTOKA KAHAMA
Katika hali isiyokuwa ya Kawaida Mkazi wa
Mtaa wa Shunu mjini Kahama, FIKIRI DAUDI (38) amejinyonga kwa kamba ya katani
usiku wa kuamkia leo baada ya kupimwa na kubainika kuishi na virusi
vya Ukimwi (VVU).
Mjane wa FIKIRI, SHIJA JULIUS amesema baada
ya kupima afya zao Mume wake alibainika kuwa na maambukizi ya VVU huku yeye
akiwa hana virusi hivyo jambo ambalo lilimkera na kuamua kuchuka uamuzi huo.
Miongoni mwa mashuhuda wa tukio hilo,
SENIFROSA DAUDI amesema taarifa za kujinyonga kwa FIKIRI zimezua majonzi
miongoni mwa wakazi wa mtaa huo.
Naye mwenyekiti wa mtaa huo, KUBE SHIJA
amewataka wananchi wa mtaa huo kuacha kuwanyanyapaa watu wenye VVU ambapo
amesema kwa mujibu wa majirani Mke wa Marehemu FIKIRI alianza kumnyanyapaa Mume
wake hali iliyosababisha achukue uamuzi huo wa kujinyonga.
SHIJA amesema mwili wa Marehemu
umechukuliwa na Jeshi la Polisi na kupelekwa katika hospitali ya Halmashauri
ya Mji wa kahama kwaajili ya Uchunguzi na baada ya hapo
watakabidhiwa ndugu kwaajili ya taratibu za mazishi.