Na
Kenneth Ngelesi, Rungwe
Umoja
wa Wakulima Wadogowadogo Nyanda za juu kusini tawi la Rungwe
(RUMBIAA)wameiomba serikali kuharakisha mpango wa kutoa hati za kimila za
kumiliki ardhi kwa wakulima hao.
Aidha
Chama hicho kimeitaka serikali kuangalia namna ambavyo fursa zinazopatikana
katika mipango yake husuasani katika suala la kilmo kwanza zinawafikia
na kuwanufaisha wakulima hao kupitia chama chao
Akizungumza
na mtandao huu wilayani hapa Mratibu wa Chama hicho Brown Mwangate mara
baada ya kikao cha kawaida ngazi ya
Wilaya ambapo mambo mbalimbali yalijadiliwa likiwemo suala la wakulima kukosa
hati miliki za kimili za umiliki ardhi.
Mwangate
alisema kuwa serikali imekuwa ikitoa
matamko mara kwa mara juu ya kutoa hati hizo kwa wakulima lakini suala hilo
limekuwa likienda kwa kasi ndogo hali inayowafanya washindwe kunufaika
na ardhi zao.
Alisema
kutokana na Wilaya hiyo kuwa na uzalishaji mkubwa wa mazao ya ndizi
pamoja na viazi na matunda hivyo kitendo cha wao kupatiwa hati hizo
kutasaidia kuongeza tija ya uzalishaji ya mazao mengine hasa kilimo cha
kahawa.
Aidha
katika hatua nyingine wakulima hao wameomba serikali kuwasaidia namna ya
kupata wawekezaji watakao jenga viwanda vya usindikaji wa matunda hasa
ndizi na mtunda kwani kuna uwezekano mkubwa wa kupata malighafi hasa
juice na biskuti hali ambayo itapunguza gharama za uagizwaji bidhaa hizo nje ya nchi.
Mratibu
huyo alisema suala jingine litakalo saidia katika hatua ya upatikanaji wa
wawekezaji ni kupunguza tatizo la ajira na kuongeza hali ya upatikanaji
wa masoko kiurahisi zaidi.