Wakati wananchi katika halmashauri za wilaya zaidi ya 55
nchini wakikabiliwa na uhaba Mkubwa wa chakula imebainika huwenda zaidi ya tani
86,222 za mahindi yaliyohifadhiwa kwenye ghala la chakula kituo cha Shinyanga
zipo katika hatari ya kuharibiwa na wadudu waharibifu
hali hiyo imeonekana baada ya kamati ya kudumu ya bunge
ya kilimo mifugo na maji kutembelea ghala hilo na kujionea jinsi mahindi
yaliyohifadhiwa hapo yalivyoharibika huku yakiwa yanatoa wadudu
Baadhi ya wajumbe hao wameiomba serikali kuangalia upya
suala la mahindi hayo yasiwe yanahifadhiwa muda mrefu wakati wananchi wakiwa
wanalalamikia suala la njaa kutokana na mvua kunyesha na badala yake wauze
mahindi hayo kwa bei nafuu
Pamoja na wajumbe wa kamati hiyo kujionea mahindi hayo
yakiwa na wadudu aina ya funza Mtendaji mkuu wa maghala ya Chakula hapa nchini
Deusdedit Mpazi amesema kuwa hali hiyo iliyopo haimaanishi kuwa mahindi hayafai
kutumika
Naibu waziri wa kilimo mifugo na Uvuvi William Ole Nasha
amekiri kuwa kuna baadhi ya wilaya ambazo wananchi wake wanakabiliwa na njaa na
serikali inatambua suala la kuwapelekea chakula cha bei nafuu linafanyika
Kamati ya bunge ya Kilimo mifugo na Uvuvi ipo mkoani
Shinyanga kwa ajili ya kukagua miradi ya maji na kujionea shughuli zinazofanywa
kupitia fedha za serikali na taasisi zisizokuwa za serikali