Licha ya Kuachiwa Huru na Mahakama, Mbunge Lijualikali arudishwa Gerezani

Mbunge wa Kilombero mkoani Morogoro ataachiwa huru baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam kutengua hukumu aliyekuwa amehukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Kilombero.

Peter Ambrose Lijualikali alihukumiwa kwenda jela kwa kipindi cha miezi sita baada ya kupatikana na hatia ya kufanya vurugu kipindi cha uchaguzi mdogo mkoani humo.

Mbunge huyo alifanya kosa hilo kipindi cha uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero mwezi Machi 2016 ambapo upinzani walilalamikia uchaguzi huo kuwa ulijawa vurugu na vitisho vya polisi.

Polisi walimkamata Mbunge huyo baada ya kudaiwa kuwa alitaka kuingia katika chumba cha kupigia kura wakati yeye hakuwa na haki ya kupigakura.

Mahakama Kilombero ilimhukumu mbunge huyo kifungo cha miezi sita jela lakini leo Mahakama Kuu imetengua hukumu hiyo baada ya mbunge huyo kuto kukutwa na hatia, na hivyo mbunge huyo ataachiwa huru.

Hata hivyo mbunge huyo amerudishwa Gerezani kutokana na kutokamilika kwa baadhi ya taratibu


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo