"Haitakiwi Kuamuru Mtumishi wa Umma Aswekwe Mahabusu"

Wakuu wa Mikoa na Wilaya wameshauriwa kutumia Busara ya kutatua migogoro ya watumishi wa serikali, badala ya kuwaweka mahabusu
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais (Tamisemi) George Simba Chawene alisema viongozi hao wanatakiwa kutumia Busara zaidi kuliko kuwakomoa watumishi pale wanapokosea kwa kuwaweka mahabusu
“Watumioshi wengi wengi wakiwemo waganga wakuu, walimu wamekuwa wakiwekwa ndani na Wakuu wa Mikoa ama Wilaya kwa madai ya kutowajibika, lakini lazima ieleweke kuwa kila mmoja majukumu yake” alisema Simbachawene
Simbachawene alisema kwa mujibu wa sheria pamoja na wakuu wa mikoa kuwa na mamlaka ya kuweka mtu mahabusu kwa saa 48 na Mkuu wa Willaya saa 24 lakini ni pale mhusika anapokuwa katika hatari ya kushambuliwa au kudhuriwa na wananchi
Alisema ingawa viongozi hao wana mamlaka ya kuwaweka watumishi mahabusu kwa muda huo, wakati mchakato wa kimahakama uwe unaendelea
“Haitakiwi kuamuru mtumishi wa Umma kuwekwa mahabusu kwa nia ya kumpa adhabu , njia nzuri ni kumhifadhi humo kwa nia nzuri kwa lengo la kumuepushia na madhara yanayoweza kumpata” alisema simbachawene.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo