Dereva Bajaji Yamfika Makubwa huko Tabora

Dereva wa bajaji mkazi wa Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora Maduhu Dwisha (37) ameuawa baada ya kukodishwa na watu wasiojulikana
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Hamisi Issa alisema Dwisha alitoweka nyumbani kwake Machi mbili akiwa amekodiwa na abiria, ambao walimuua na kutokomea na bajaji hiyo na kuutelekeza mwili wake ambao ulipatikana Machi 4 mwaka huu
Kamanda Issa alisema kutokana na Mauwaji hayo jeshi la polisi linaendelea kuwatafuta wauwaji pamoja na Bajaji iliyoporwa 
Kamanda aliongeza kuwa kutokana na mauwaji kuongezeka siku za hivi karibuni jeshi la polisi linampango wa kuweka muda maalumu kwa madereva wa bajaji kufanya kazi zao usiku

Akizungumzia tukio hilo Mke wa marehemu Mwadawa Jumanne (32) alisema mumewe alitoweka tangu machi 2 saa nane mchana na kwamba alimtafuta kupitia simu yake ya mkononi bila mafanikio, hadipale alipokuja kupata taarifa kuwa mumewe ameuawa na majambazi


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo