Afisa Mtendaji wa kijiji hicho Bw. Kayanda Chengula
amefikia uamuzi huo baada ya kutolewa kama kero katika mkutano wa hadhara,
ambapo mwananchi mmoja amesema katika matukio ya wizi yaliyotokea katika kijiji
hicho hivi karibuni, watuhumiwa wamekuwa ni wageni waliofika kijini hapo bila
kufuata taratibu
Akijibu hilo Afisa mtendaji huyo wa kijiji akawaagiza
wenyeviti wa vitongoji waorodheshe majina ya wageni na wanakotoka na wafike nao
katika ofisi za kijiji ambapo watapatiwa utaratibu
Pia mtendaji huyo ameelezea ni kwa nini amekuwa na
utaratibu wa kutumia mgambo kuwakamata watuhumiwa badala ya kutoa taarifa ya
wito wa kufika ofisini maarufu kama "samasi" Kuwa inatokana na aina
ya kosa alilolifanya mtuhumiwa
Katika hatua nyingine Afisa Mtendaji wa kata ya Lupalilo
Bi. Bertha Adelberth amewasisitizia wananchi hao kujenga vyoo bora licha ya
kuwepo kwa changamoto ya maji, na kwamba wakati wananchi wakiendelea kujenga
vyoo hivyo wao kwa upande wao watahakikisha wanashirikiana na serikali
kufikisha maji katika maeneo yote ya kata hiyo
Wakati huo huo Afisa kilimo na Mifugo kata ya Lupalilo
Bw. Festo Mwansanga amewataka wananchi waliopanda miti kwenye mashamba ya
kilimo na maeneo ya kuchungia mifugo kuanza kuiondoa wenyewe kwa kuwa sheria na
mikakati ya halmashauri ya wilaya ya Makete kwa sasa hairuhusu hali hiyo