Muonekano wa daraja la barabara ya kwenda Kiguru kama ilivyopigwa na mtandao huu mwaka 2013
Serikali imepongezwa kwa kufanikisha uwepo wa barabara
katika Kata ya Kiguru wilayani Makete mkoani Njombe ambapo kwa mara ya kwanza
mwaka huu Gari limeweza kufika katika kata hiyo
Akizungumza na mwandishi wetu katika mahojiano maalum
Diwani wa kata ya Kiguru Mh Simon Mwaikenda amesema wananchi wa kata hiyo
wamekuwa wakipata tabu kufuata huduma mbalimbali hasa za matibabu kwa kuwabeba
wagonjwa kwenye machela kwa umbali mrefu mpaka halmashauri ya Busokelo mkoani
Mbeya kupata huduma za hospitali
Amesema wazo la kuanzisha barabara ya kwenda katika kata
yake lilianza mwaka 1958 na mafanikio yameonekana mwaka huu wa 2017 ambapo
barabara imekamilika na kupitika kwa gari mpaka kwenye kata hiyo
Kufuatia kukamilika kwa barabara hiyo ameelezea kutakuwa
na manufaa na kufungua fursa za kiuchumi na maendeleo katika kata hiyo, pamoja
na uharaka wa kuwapeleka wagonjwa ama kina mama wajawazito kupatiwa matibabu ya
rufaa nje ya zahanati ya kijiji chao, ambapo ni hospitali zilizopo halmashauri
ya Busokelo wilayani Rungwe mkoani Mbeya
Amesema wananchi walijawa na furaha kuona gari kwa mara
ya kwanza limefika katika kata hiyo tangu ianzishwe, na kuipongeza serikali kwa
jitihada hizo za kufanikisha utatuzi wa kero hiyo ya muda mrefu
Sikiliza sauti hapa chini:-
Sikiliza sauti hapa chini:-