Baraza la Madiwani wa
Halmashauri ya wilaya ya Makete mkoani Njombe Limepokea taarifa ya Tume ya
Uchunguzi iliyoundwa na Mkurugenzi mtendaji kuchunguza suala la uuzwaji wa
msitu wa Iwawa na wa Nungu inayomilikiwa na halmashauri
Kuundwa kwa tume hiyo
kulitokana na madiwani hao kutoridhika na mapato yaliyotokana na uuzwaji wa
misitu hiyo na kusababisha watumishi kadhaa kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi
mwishoni mwa mwaka jana
Taarifa hiyo ya uchunguzi
imepokelewa baada ya Baraza hilo kujigeuza kama kamati na baada ya majadiliano
yakatolewa maamuzi, ambapo baraza limepongeza kazi iliyofanywa na tume lakini
limebaini mapungufu kidogo katika taarifa
Akitoa taarifa kwa baraza
hilo Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete Mh. Egnatio Mtawa amesema
wameunda timu ya watu wanne ambao ni madiwani kwenda kushughulikia mapungufu
yaliyojitokeza katika taarifa ya tume na mwishowe yapelekwe kwenye kamati ya
fedha na mipango kabla ya kuletwa upya kwenye baraza hilo
Wakati huo huo baraza hilo
baada ya kujigeuza kama kamati limepitisha ombi la kuthibitishwa kwa wakuu
wawili wa idara na wawili wa vitengo ambapo Bw. Raisi Tembo amethibitishwa kuwa
mkuu wa Idara ya Ujenzi, Bw. Aldo Mwapinga kuwa mkuu wa Idara ya Mifugo na
Uvuvi, huku Bw. Gregory Emmanuel akithibitishwa kuwa mkuu wa kitengo cha
Uchaguzi na Bw. Sebastian Mukhondya akithibitishwa kuwa mkuu wa kitengo cha
Ugavi
Katika hatua nyingine kwa
sasa wilaya ya Makete inakabiliwa na upungufu wa walimu zaidi ya 200 kwa shule za
msingi wilayani hapa
Hayo yamesemwa katika baraza
la madiwani na Afisa elimu Msingi Mwl Antony Mpiluka ambapo amesema miongoni
mwa sababu zilizochangia upungufu huo ni zoezi la uhakiki watumishi hewa,
pamoja na kutopata walimu wa ajira mpya kwa miaka mitatu mfululizo