Taarifa zilizotufikia Hivi Punde Kutoka Ofisi ya Mbunge wa Mikumi

Mkulima mmoja aitwaye OMARY SULULU mapema Leo tar 1 January 2017 ameshambuliwa na kujeruhiwa vibaya kwa kukatwa na panga kichwani na mfugaji kwenye kijiji cha MAMOYO kata Ya MABWEREBWERE Jimbo La Mikumi.

 Tukio hilo limetokea baada ya Ndugu OMARY SULULU  alivyokuwa akijaribu kufukuza mifugo hiyo kwenye mashamba ya Migomba, nyanya na Mahindi,  Kwa sasa Ndugu OMARY SULULU anaendelea na Matibabu katika Hospitali Ya Wilaya Ya Kilosa.

Juhudi zilizokwishafanywa na Mhe Mbunge  ameweza kuwasiliana na Mkuu wa Wilaya Ya Kilosa kwa hatua zaidi

Lakini pia Mbunge wa jimbo La Mikumi Mhe JOSEPH LEONARD HAULE anaendelea kutoa wito na kuiomba sana serikali itusaidie kutatua migogoro hii isiyokwisha ya wakulima na wafugaji wilayani KILOSA...


Imetolewa na:~

Robert A. Galamona
Katibu Ofisi Ya Mbunge
Jimbo La Mikumi


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo