Uongozi wa mkoa wa Tabora umemsimamisha kazi mara moja na kuagiza hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake, muuguzi katika kituo cha afya cha Mazinge wilayani Sikonge, baada ya kubainisha kuelekea kumsababishia kifo mtoto wa miaka tisa aliyekuwa amewekewa dripu ya maji na kuamua kumchomolea bila sababu.
Katibu tawala Dr.Thea Ntara aliyefika katika kituo hicho na kupata malalamiko dhidi ya muuguzi huo, Bi. Zaituni Lai, ameamua kuchukua hatua hiyo kwa lengo la kuweka nidhamu katika vituo vya afya na hospitali ili watoa huduma wawathamini wananchi wanapokwenda katika hospitali.
Akitekeleza agizo hilo mkuu wa wilaya ya Sikonge Bw.Peres Magiri, ameliagiza jeshi la polisi kuhakikisha linamshikiria muuguzi huyo, mpaka hatua ya mwisho ya maagizo ya serikali ya mkoa wa Tabora yatakapokamilia kwa hatua za kinidhamu.