Waziri Mkuu mstaafu na aliyekuwa mgombea urais kwa CHADEMA Mh. Edward Lowassa na mbunge wa Geita (M) Viti maalum Upendo Peneza wamekamatwa na jeshi la Polisi Geita mjini.
Taarifa zinaarifu kuwa Lowassa amefika Geita leo akitokea Kagera ambapo alipofika stendi ya zamani Geita wananchi walimsimamisha. Aliposhuka kwenye gari kuwasalimu wanageita, polisi wakamkamata na kumpeleka kituo cha Polisi Geita.
Lowassa alikuwa anaenda kwenye kampeni za uchaguzi Kata ya Nkome
Katika sakata hilo waandishi nao wakapokea kipigo kutoka kwa askari polisi wakiwazuia kutofanya majukumu yao na baadhi ya vifaa vyao kutupwa chini.
Lowassa alikuwa anaenda kwenye kampeni za uchaguzi Kata ya Nkome
Lowassa amekamatwa akiwa na viongozi wengine ambapo alikuwa ameambatana na mbunge viti maalumu kwa tiketi ya Chadema Upendo Peneza, Mwesiga Baregu, na mkurugenzi wa oganaizesheni ya mafunzo wa Chadema Singo Benson.
Hata hivyo Lowassa aliachiwa Baadaye baada ya kubainika kuwa lengo la kumkamata lilikuwa ni kuokoa hatari ambayo angeweza kuipata na hadhi yake ya kiuongozi kwa taifa kutoka kwa umati wa watu uliokusanyika kumzingira