Kiwanda cha Takataka Kujengwa Dar

Na Elvan Stambuli
MEYA wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Samwel Sitta amesema manispaa yake itajenga kiwanda cha kuchakata takataka na kutoa ajira ya zaidi ya watu 500 mwaka huu.
Akifanya mahojiano na Global TV Online Bamaga Mwenge Dar leo, Meya Sitta alisema mchakato wa kupata kiwanda hicho umekamilika na kinafadhiliwa na Wajerumani wa Mji wa Humburg.
“Takataka zitakuwa ni fedha kama zilivyo chupa za plastiki. Kutakuwa na magari ambayo yatakuwa yakikusanya takataka mjini na kwenda kuyasindika kuwa mbolea kwenye kiwanda Mabwepande. Kuna faida nyingi za mradi huo kwani mji utakuwa safi na pili vijana watapata ajira,” alisema Meya Sitta.
Alisema licha ya kiwanda hicho, kuna mpango katika manispaa yake kuboresha makazi ya watu kama vile Tandale, Mwananyamala na Uwanja wa Fisi, Manzese ambako kutajengwa maghorofa ya kisasa baada ya makubaliano na wananchi wa maeneo hayo na manispaa yake.
Picha na Musa Mateja/GPL


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo