Mkuu wa Wilaya ya Makete Veronica Kessy

HERI YA MWAKA MPYA!
Ndugu wananchi wa Makete na Watanzania wote kwa ujumla,wananchi wa kijiji cha Isapulano katika kata ya Isapulano hapa Wilayani Makete wamepatwa na maafa mnamo tarehe 02/01/2017
Maafa hayo yalisababishwa na mvua kubwa iliyoambatana na upepo,jumla ya nyumba 16 zenye jumla ya watu 37 ziliathirika kwa viwango tofauti
Katika tukio hilo waliumia watu wawili,wakapatiwa matibabu katika Zahanati ya Isapulano na kwa bahati nzuri wanaendelea vizuri,Aidha tunamshukuru Mungu hakuna mwananchi aliyefariki
Ndugu wananchi nyumba hizo zinahitaji vifaa vya ujenzi yaani matofali, saruji, mbao, misumari, mabati n.k, pia wananchi walioathirika wanahitaji kusaidiwa mahitaji ya kibinadamu kwa hiyo nawaomba wananchi na wadau wote wa ndani na nje ya Wilaya ya Makete tuguswe kwa namna moja ama nyingine kuchangia fedha au vitu ili kuwasaidia wananchi hao
Kwa sasa wananchi hao wamehifadhiwa na majirani na ndugu zao,Aidha wananchi wa kijiji hicho wameanza kujitolea kusaidia ujenzi huo
Ninawashukuru na kuwapongeza kwa jitihada hizo,nawasihi tuwaunge mkono kwa kutoa misaada ya hali na mali,michango ya fedha iingizwe kwenye Akaunti ifuatayo iliyopo NMB MAKETE
Jina la Akaunti:Kijiji cha Isapulano
Namba ya Akaunti:60410004408
Na msaada wa vitu au vifaa uwasilishwe kwa Mtendaji wa kata ya Isapulano Bi.Tabu Mohamed mwenye namba 0745571046
Sikiliza sauti yake hapa chini:-