Nyumba za NHC zilizojengwa Ngiu Makete
Msafara wa naibu waziri ukiwasili katika nyumba hizo
Naibu waziri wa ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi Mh
Anjelina Mabula ameishauri jamii na wadau mbalimbali wa maendeleo kujitokeza
kununua nyumba zinazojengwa na shirika la nyumba la taifa NHC zilizopo eneo la
Ngiu Makete mjini wilayani hapo
Naibu waziri ameyasema hayo leo katika ziara yake ya
kikazi aliyoifanya wilayani hapo ambapo mbali na kuzungumza na wananchi katika
mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Tandala wilayani Makete, pia ametembelea
ujenzi wa nyumba hizo zipatazo 30 ambao upo katika hatua za mwisho za
umaliziaji
Amesema kwa sasa maisha ni nyumba hivyo wananchi
wakijitokeza kununua nyumba hizo kutasaidia serikali kupata fedha ambazo
zitawezesha nyumba nyingine kujengwa katika maeneo mbalimbali ya nchi ili
huduma hiyo iwafikie wananchi wengi wenye lengo la kuwa na makazi bora
Awali akizungumza mbele ya naibu waziri mhandisi wa
ujenzi kutoka shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw Edward John ameelezea hatua za
ujenzi huo kwa kusema kuwa nyumba 30 zipo katika hatua za mwisho za umaliziaji
wa ujenzi wake ambapo zinatarajiwa kumalizika hivi karibuni
Naye meneja mauzo wa NHC Bw. Erasto Chilambo amesema
tayari wameshafanya matangazo ya kutosha kuhusu ununuzi wa nyumba hizo, na
gharama za kuuza nyumba moja ni Zaidi ya shilingi milioni 54 za kitanzania
pamoja na VAT na shilingi milioni 46 bila VAT
Sikiliza sauti hapa chini:-