Yametimia, Rais Magufuli Kufanya ziara Kwa Waathirika wa Tetemeko Kagera

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.John Pombe Magufuli anatarajia kuwasili mkoani Kagera ambapo atafanya ziara ya siku mbili yenye lengo la kuwatembelea wananchi walioathirika na tetemeko la ardhi, kukagua na kuweka mawe ya msingi katika miradi katika baadhi ya inayojengwa upya baada ya kuharibiwa na tetemeko.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake leo mkuu wa mkoa wa Kagera meja jenerali mstaafu Salum Mstapha Kijuu amesema Dkt.Magufuli atawasili kesho asubuhi mkoani Kagera akitokea mkoani Geita na baadae atahudhuria ibada ya misa na kesho yake atawatembelea baadhi ya wananchi waliotumia zao kujenga upya nyumba zao za makazi zilizoharibiwa na tetemeko na atatembelea mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari ya ihungo na kuweka jiwe la msingi na baadae kuzungumza na wananchi katika eneo la shule hiyo. 

Mkuu huyo wa mkoa amewaomba wananchi katika mkoa huo wajitokeze kwa wingi kumpokea Dkt.Magufuli na kuwahimiza waendelee kudumisha amani, utulivu, mshikamano na upendo kama kawaida yao pia amewaasa wajiepushe na vitendo vya uvunjifu wa amani. 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo