Waziri akataa barabara iliyojengwa chini ya kiwango

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama ameikataa barabara ya changarawe ya Kitanda mpaka Namatanda iliyopo wilaya ya Namtumbo, mkoani Ruvuma iliyojengwa chini ya kiwango.

Waziri Mhagama amefikia hatua hiyo katika ziara yake kuangalia maendeleo ya miradi inayosimamiwa na ofisi ya Waziri Mkuu wilayani humo ambapo amegundua kuwa moja ya daraja katika barabara hiyo halina ubora.

Amesema kutokana na ujenzi huo uliokuwa chini ya kiwango, kuna uwezekano msimu mmoja wa mvua daraja hilo likasombwa na maji na hivyo kuagiza mapungufu yaliyopo yarekebishwe.

Katika ziara hiyo Waziri Jenista ametembelea mradi wa kilimo cha mpunga ambapo Katibu wa Mradi huo wa Umoja wa Wakulima wa Umwagiliaji katika kijiji cha Kitanda, Melkiol Mango amesema kuna ongezeko la wanachama kutoka 12 walipoanza umoja  huo mwaka 2000 na 105 hivi sasa.  


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo