Makubwa: Wajiuzia viwanja uwanja wa ndege Mbeya

Uwanja wa ndege wa Mbeya
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini -TAA imesema watu waliojimilikisha na kupima viwanja katika Uwanja wa Ndege wa Mbeya hawakuishirikisha wala kuruhusiwa na Mamlaka hiyo.

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa TAA, Lawrent Mwigune amemweleza mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makala kuwa uuzwaji wa viwanja ndani ya uwanja wa ndege wa Mbeya, unafanyika kimakosa.

Kufuatia hali hiyo Mkuu wa mkoa wa Mbeya ameuagiza uongozi wa mamlaka ya viwanja vya ndege  nchini  kukutana na watu waliouziwa viwanja vya makazi ndani ya uwanja huo wa ndege wa Mbeya na kutoa maelezo kamili  juu ya viwanja  vilivyopimwa  kwa ajili ya makazi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo