
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
Rais amesema kuna ‘wapiga deal’ walikuwa wameingilia mradi wake huku Dangote akisema mwezi huu analeta malori 600 kwaajili ya shughuli zake na kubebea saruji na kwamba atanunua kila rasilimali kwaajili ya kiwanda hicho hapa hapa Tanzania. Pia amedai kuwa atatengeneza ajira zingine mpya zaidi ya 1,500.