Lowassa, Maalim Seif wampa pole Mbatia

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, wamekwenda kumjulia hali Mwenyekiti wa NCCR–Mageuzi, James Mbatia baada ya kutoka kwenye matibabu nchini India, ambako alifanyiwa upasuaji wa mguu.
lowassa-na-maalim-seif-2
Mbatia, ambaye pia ni Mbunge wa Vunjo, alifanyiwa upasuaji huo Novemba 14 katika Hospitali ya Zydus Ahmedabad Gujarat baada ya mguu huo kumsumbua kwa takribani miaka 37.
Lowassa akiwa nyumbani kwa Mbatia Mbezi amesema, “Nimekuja kumuona mheshimiwa (Mbatia). Nimefurahi zaidi baada ya kunieleza anaendelea vizuri. Watanzania waendelee kumuombea na siku zijazo atazidi kupata nafuu zaidi.”
Maalim Seif alimpa pole na kusema, “Binadamu ndivyo tulivyoumbwa, kuna kuumwa na usipoumwa tushukuru Mungu.”
Akizungumzia matibabu yake, Mbatia alisema ilitumika teknolojia ya kisasa kwenye upasuaji huo uliochukua saa nne kutokana na tatizo la mguu lililoanza akiwa na umri wa miaka 15.
Chanzo:Mwananchi


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo