MAGARI ya abiria yanayofanya safari zake kati ya Kamsamba na Mlowo mkoani Songwe jana yalikumbwa na wakati mgumu kiasi cha kusitisha safari zake kwa muda kutokana na maji ya mitaro yaliyotokana na mvua kubwa sambamba na utelezi kuhatarisha usalama wake na abiria.
Kwa ujumla barabara ya Kamsamba hadi Mlowo ambayo ni ya changarawe, imeendelea kuathiriwa na maji yanahoporomoka kwa kasi na kuondoa vipande vya barabara pembezoni hivyo kupunguza upana wake.
Pichani moja ya mabasi yanayofanya safari eneo hilo lilisimama kwa takriban saa 2 kusuburi maji yapungue ndipo liendelee na safari baada ya mkondo wa maji ya mvua kumega sehemu ya barabara na hivyo kuhatarisha usalama wa magari yanayopita eneo hilo
Chanzo:Mbeya yetu blog


