Atakayepoteza mtoto mwaka mpya kukamatwa

Wazazi na walezi mkoani Mtwara wametakiwa kuwachunga watoto wao katika sherehe za sikukuu ya mwaka Mpya, na kwamba atakaepotelewa na mtoto kwa uzembe atachukuliwa hatua za kisheria.

Wito huo umetolewa mkoani humo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Thobias Sedoyeka na kuongeza kuwa jeshi hilo halitokuwa na huruma kwa mzazi yeyote atakayetelekeza mtoto wake.
Jeshi hilo limeendelea kutoa tahadhari za kiusalama kwa watumiaji wa vyombo vya moto kuhakikisha wanakuwa waangalifu na kuepuka kuendesha vyombo vyao wakiwa wamelewa, pamoja na kuwataka wafanyabiashara wa bar kuhakikisha wanafunga biashara zao katika muda uliopangwa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo