Mwandishi wa habari wa ITV akamatwa kwa amri ya DC

Mwandishi wa habari wa ITV mkoani Arusha Bw Khalifa Lihundi anashikiliwa na polisi kituo cha Usa River wilayani Arumeru mkoani Arusha kwa tuhuma za kuandika habari za zinazodaiwa kuwa ni za uchochezi.

Bw Lihundi amekamatwa jijini Arusha majira ya saa nane mchana na  askari anayedaiwa kutumwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru Bw  Alexsander Mnyeti kama alivyoeleza Bw Basili Elias ambaye alishuhudia  tukio hilo.

Akizungumzia suala hilo mpiga picha wa Bw Khalifand Lihundi Bw   Deogratius Kassamia amesema habari inayodaiwa kuwa ni ya uchochezi ilikuwa ni ya malalamiko ya wananchi juu ya tatizo la maji.

Akizungumzia tukio hilo mwenyekiti wa chama cha waandishi wa  habari mkoa wa Arusha Bw Cloud Gwandu pamoja na kulaani kitendo  hicho amesema hatua hiyo haikubaliki kwani haikufuata taratibu.

Taarifa zaidi zimeeleza kuwa huenda Bw Lihundi akafikishwa  mahakamani hapo kesho.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo