Msanii Dogo Janja apata Msiba Mzito

Msanii wa muziki wa hip hop kutoka Tip Top Connection Dogo Janja amefiwa na baba yake mzazi, Abubakari Chande.
jjkk
Mzazi wake huyo ambaye alikuwa akiishi mkoani Arusha, ni mmoja kati ya watu wake wa karibu ambao walikuwa wanamshauri katika muziki wake.
Kupitia instagram, Dogo Janja ameandika:
PUMZIKA KWA AMANI BABA YANGU KIPENZI.😭 Hakika MUNGU Amefanya Maamuzi Yake Siwezi Kukufuru Zaidi Ya Kukuombea kwa ALLAH akupe kauli Thebeet! Umelala baba yangu sitakuona tena😭 EEH MWENYEZI MUNGU UMPOKEE,UMUONDOLEE ADHABU ZA KABURI. Lala baba hakika wote njia yetu ni moja.. siku moja tutaonana tena baba! R.I.P Kamanda ABUBAKARI CHENDE!
Kiongozi wa Tip Top Connection, Babu Tale amempa pole rapa huyo.
“Pole Dogo Janja Mungu akutie nguvu katika kipindi hiki kigumu na amuweke Baba katika njia inayo stahiki,” aliandika Babu Tale instagram.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo