Mkuu wa wilaya ya Ludewa mkoani Njombe Mh Patrick Tsere
amekemea tabia ya ushirikina inayoelekezwa kwa baadhi ya walimu wilayani mwake
kwani inachangia kurudisha nyuma maendeleo ya elimu
Mkuu huyo wa Wilaya ametoa kauli hiyo wakati akitoa mchango
wake kuhusu sekta ya elimu katika kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa (RCC)
kilichofanyika leo mkoani Njombe, ambapo amesema pamoja na jitihada
zinazofanywa na serikali kuboresha elimu bado wapo wanajamii wanaowatisha
walimu na wengine kudiriki kuwafanyia vitendo vya kishirikina vinavyosababisha
walimu kukimbia ama kuondoka na kuacha kufanya kazi hiyo
Amesema wakishaondoka inapelekea wilaya na mkoa kwa ujumla
kuwa na upungufu mkubwa wa walimu ili hali jambo hilo halitakiwi kufanywa na
wanajamii badala yake washirikiane na walimu kuleta maendeleo ya elimu kwa
manufaa ya watoto wao na taifa kwa ujumla
Pia mkuu huyo wa wilaya ameshangazwa na baadhi ya wabunge wa
mkoa wa njombe kulalamika katika kikao hicho kuhusu kuchelewa kwa pembejeo za kilimo,
na kusema hawatakiwi kushangaa kwa kuwa wao ndio walipitisha bajeti ya wizara
hiyo na kwa nini hawakushikilia shilingi ya bajeti hiyo
Amesema malalamiko yao katika kikao hicho hayasaidii badala
yake waongee na waziri wa kilimo moja kwa moja kumweleza changamoto za wilaya
zote za mkoa wa Njombe kuhusiana na kilimo kwa kuwa kila wilaya ina changamoto
zake, hivyo pembejeo kuchelewa bado linaendelea kujitokeza licha ya maazimio ya
vikao mbalimbali kuazimia pembejeo zisicheleweshwe
Sikiliza sauti zake hapa chini:-