Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Theophil Makunga (kulia) na Mtaalamu Mshauri Rosemary Mwakitwange wakiangalia mada zitakazo jadiriwa katika mkutano huo.
Wahariri Idrisa Jabir na Charles Mwankenja (kulia), wakijadili jambo.
Na Dotto Mwaibale
WAHARIRI wa vyombo vya habari wamekutana katika mkutano maalumu wa siku mbili kwa ajili ya kujadili mambo kadhaa yanayohusu tasnia hiyo nchini.
Akizungumza wakati akifungua mkutano huo Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Theophil Makunga alisema mkutano huo utawajumuisha wadau wa sekta ya habari kutoka ndani na nje ya nchi.
"Tumewaalika wenzetu wa nje ili watupe uzoefu wa jinsi wanavyofanya katika tasnia ya habari katika nchi zao" alisema Makunga.
Alisema katika mkutano huo ambao unafanyika Hoteli ya Protea Court Yard mambo yatakayo zungumziwa ni kupitia sheria ya huduma ya vyombo vya habari iliyopitishwa na Bunge na kusainiwa na Rais Dk. John Magufuli pamoja na kujadili mpango mkakati wa Jukwa la Wahariri wa kuendeleza tasnia ya habari nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Habari Tanzania (TMF), Ernest Sungura alisema ni muhimu kwa wanahabari kuwa na mpango mkakati wa miaka 10 ili kupata majibu sahihi ya tasnia hiyo.