Mshambuliaji wa timu ya vijana ya Mbao Fc U-20 Ismail Mrisho Khalfan anayevalia jezi nambari 4 amefariki dunia jioni hii baada ya kuanguka Uwanjani Kaitaba mjini Bukoba wakati wa Mtanange wao dhidi ya timu ya vijana wa Mwadui ikiwa ni mechi ya mwisho ya kumaliza duru la kwanza la ligi ya Vijana. Ismail Mrisho Khalfan amefariki akiwa na miaka 19.
Mshambuliaji wa timu ya vijana ya Mbao Fc U20 Ismail Mrisho Khalfan anayevalia jezi nambari 4 amefariki Dunia jioni hii baada ya kuanguka Uwanjani Kaitaba wakati wa Mtanange wao dhidi ya timu ya vijana wa Mwadui ikiwa ni mechi ya mwisho ya kumaliza duru la kwanza la ligi ya Vijana.
Ismail Khalfan amefariki akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Mjini Bukoba.
Mrisho Halfan ndie aliyeifungia bao la kwanza na bao la pili lilifungwa kwa mkwaju wa Penati hivyo mtanange kumalizika kwa 2-0.
Hivi ndivyo mtanange ulivyokuwa Uwanjani Kaitaba jioni hii.
Ismail Mrisho Khalfan ndiye aliyeifungia bao la kwanza Mbao FC. Na hapa akishangilia bao lake la kwanza kwa aina yake kwa Timu ya Mbao Fc
Shangwe!
Ismail Mrisho Khalfan(kulia)
Vijana wa Mbao Fc walianza kipindi cha kwanza wakiwa kwenye hali ya kutaka kuibuka na ushindi
Ismail Mrisho Khalfan(kulia) akimkacha mchezaji wa Mwadui fc.
Picha zote na Faustine Ruta, Bukoba