Watuhumiwa 15 wakamatwa Arusha Kwa Wizi wa Umeme

Maafisa wa shirika la umeme Tannesco mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na jehi la polisi wamefanya msako wa wezi wa umeme usiku wa manane katika mitaa ya jiji la Arusha na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa kumi na tano walio jiunganishia umeme kinyume na taratibu.

Akizungumza katika operesheni hiyo mdhibiti mapato wa tanesco mkoani  arusha Mhandisi Hasani Juma amesema wamegundua zaidi ya nyumba mia moja zimeunganishwa umeme wa wizi na mbaya zaidi wameunga kutoka njia kuu na kupitisha kwenye miti ambayo ni hatari kiusalama.

Afisa mahusiano huduma kwa wateja Tanesco mkoa wa Arusha Fredy Robati amesema wamelazimika kufanya opereshani hiyo usiku wa manane ili kudhibiti wizi huo.

Baadhi ya watuhumiwa wa wizi wa umeme waliokamatwa wamekiri kutumia umeme huo kwa njia ya wizi kwa kuunganishiwa na watu waliyojitasmbuulisha kuwa ni maafisa wa shirika hilo kwa malipo ya shilingi elfu tano kwa mwezi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo