Wakati Lema akipelekwa mahabusu kusubiri Hatima ya dhamana yake siku ya Ijumaa tarehe 11 November 2016 baada ya kusomewa mashitaka ya uchochezi ameondoka akiwa na Bibilia ambayo maadiko yote yapo katika Bibilia Takatifu
;;;;;;
Mbunge wa Arusha Mh Godbles Lema amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu mkazi mkoa wa Arusha na kusomewa shitaka la uchochezi na maneno ya kashfa dhidi ya viongozi wa serikali akiwemo Mh Rais Dk.John Magufuli na kisha kupelekwa gerezani baada ya kunyimwa dhamana.
Baada ya mh lema kufikishwa katika mahakama hiyo chini ya ulinzi mkali mh Lema alisomewa shtaka la kosa hilo analodaiwa kulitenda katika maeneo mbalimbali na kwa nyakati tofauti mbele ya hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo Desder Kamugisha.
Akiwa mahakamani hapo wakili wa serikali mwendesha mashtaka wa serikali aliiambia Mahakama hiyo kuwa Mh Lema alitenda kosa hilo tarehe 22/10 2016 Mh Lema akiwa katika eneo la kambi ya fisi kata ya Ngarenaro,kosa ambalo pia alilirudia katika mikutano mingine ukiwemo uliofanyika katika kata ya Baraa.
Baada ya kusomewa shtaka hilo Mh Lema alikana na ndipo ukafika muda wa mawakili wake kuomba dhamana ambayo hata hivyo ilikataliwa na upande wa walalamikaji ambao ni wakili wa seikali kwa madai kwamba Mh Lema awali alikuwa na kesi nyingine mbili katika Mahakama hiyo na alipopewa dhamana alifanya tena makosa kwa nyakati tofauti.
Hali hiyo iliibua mvutano wa mawakili wa pande zote,huku mawakili wa upande wa Lema ulioongozwa wakili John Malya lakini hadi mwisho Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo Desderi Kamugisha alikubali ombi la wakili wa serikali la kukataa dhamana na kudai kuwa anataka apate muda wa kujiridhisha na akaahidi kuwa atatoa uamuzi kukubali ama kuendelea kukataa dhamana siku ya Ijumaa tarehe 11/11/2016.
Baada ya maamuzi hayo Mh Lema alipandishwa kwenye Karandinga na kupelekwa magereza tukio ambalo liliibua hali ya taharuki kwa baadhi ya wafuasi wake waliokuwa mahakamani hapo ambao hawakutarajia huku wakili wake John Malya akisema kuwa watasubiri kuona maamuzi yatakayotolewa siku hiyo ya Ijumaa.
Hii ni mara ya pili kwa Mbunge huyo wa Jimbo la Arusha Mh Godbless Lema kupelekwa magereza katika kipindi chake cha miaka sita ya ubunge huku akiwa ameshakamatwa na kuhojiwa na kufikishwa mahakamani mara kadhaa kutokana na madai ya makosa mbalimbali ya kisiasa .