Msajili:Haiwezekani watumishi wa umma kuiba fedha za kwenye akaunti maalum

Msajili wa Hazina,
Lawrence Mafuru amesema haiwezekani kwa watumishi wa umma kuiba fedha zinazowekwa kwenye fixed deposit accounts(akaunti maalum) kwa sababu miamala ya benki ni ya uwazi.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam, Mafuru alisema hizo ni tuhuma tu na Serikali imemwagiza CAG kuchunguza.

"Nimefanya kazi kazi kwenye taasisi za benki kwa miaka 20, sijawahi kuona watumishi wa umma wakichota hela kwenye fixed deposit account

Pale kwenye benki kuna miamala ya aina mbili tu, ya kuweka na kutoa. Usipoweka wazi wakati wa kuweka, siku utakapozitoa itaonyesha tu," alisema Mafuru.

Alisema hakuna kosa kwa taasisi za serikali kuweka fedha kwenye akaunti hizo, lakini serikali sasa imeamua kuzihamishia BOT ili iwe rahisi


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo