Jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani limekamata mabasi matatu yanayofanya safari zake mikoani na moja nje ya nchi na madereva wake kuwekwa maabusu baada ya kukiuka sheria za usalama barabani.
Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa kipolisi Kinondoni Theopista Mallya amesema mabasi hayo yalikuwa yanakwepa kukaguliwa kwa kutokuingia kituo kikuu cha mabasi Ubungo na baada ya kukaguliwa yamekutwa na makosa mbalimbali ikiwemo ubovu.
Aidha amesema madereva hao watafikishwa mahakamani ili iwe fundisho kwa wengine hasa msimu huu wa sikukuu huku akiwataka wamiliki na madereva wa mabasi kufuata taratibu na sheria kwani hawatasalimika.