Mbunge wa Arusha Mjini Godbles Lema ambaye alishtakiwa kwa kosa la kutoa maneno ya uchochezi dhidi ya viongozi wa serikali, leo November 11.2016 amefikishwa mahakamani ambapo hata hivyo amenyimwa dhamana kutokana na sababu mbalimbali.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Arusha zinaeleza kuwa, katika kesi hiyo leo watu mbalimbali walifurika kwa wingi nje ya Mahakama hiyo huku ulinzi mkali ukiimalishwa ndani na nje ya viunga vya Mahakama hiyo.
Taarifa zinaeleza kuwa, Lema amenyimwa dhama kwa sababu ya Usalama wa Rais na wake mwenyewe hata hivyo baada ya dakika kadhaa kurejea kwa Hakimu, na kuamuru dhamana aliyoruhusu itenguliwe mpaka hapo itakapoamuliwa vingine.
Lema amerejeshwa tena mahabusu mpaka hapo kessi hiyo itakapotajwa tena.
Taarifa zaidi zitawajia punde.
Mbunge wa Arusha Mh. Godbless Lema akiwapungia mikono wafuasi wake wakati wa kutoka nje ya Mahakama Arusha akirejea Mahabusu leo Novemba 11.2016
Ulinzi ukiwa umeimalishwa nje ya Mahakama hiyo
Basi la Magereza likiondoka Mahakamani hapo
Baadhi ya wananchi waliofurika kwa wingi kushuhudia kesi hiyo
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi