Jumla ya wanafunzi 10 wa shule ya sekondari
Mang'oto Kata ya Mang'oto wilayani Makete mkoani Njombe wamejeruhiwa na radi
baada ya Mvua iliyoambatana na radi kunyesha shuleni hapo na kuwapiga wanafunzi
hao
Akizungumza na Mwandishi wa eddy blog shuleni hapo Mkuu
wa shule hiyo Mwl. Bonaventura Mgaya (pichani juu) amesema tukio hilo limetokea Oktoba 30
mwaka huu majira ya saa saba na nusu mchana wakati wanafunzi wakipata chakula
cha mchana shuleni hapo
Amesema radi hiyo ilivyopiga wanafunzi wengi
walidondoka chini hali iliyowafanya walimu kwenda kuwasaidia na baada ya dakika
chache baadhi yao waliweza kuzinduka ndipo walimu walipofanya uchunguzi wa
awali kugundua majeruhi na kuwakimbiza kupata huduma za afya katika zahanati ya
Mang'oto
Uchunguzi wa wataalamu wa afya katika zahanati
hiyo ulibaini mtoto mmoja kujeruhiwa zaidi upande wa kulia wa mwili wake
kuanzia begani mpaka mapajani na kulazimika uongozi wa shule kumkimbiza mpaka
hospitali ya Consolata Ikonda kwa matibabu zaidi, kabla ya baadaye wanafunzi
wengine watatu walioonekana awali kuwa walikuwa na nafuu walizidiwa na
kukimbizwa tena katika hospitali hiyo kwa matibabu zaidi
Mwalimu Mgaya pia amezungumzia madhara mengine
yaliyotokana na radi hiyo kuwa ni kuunguza mfumo wa umeme wa sola uliokuwa
ukitumika shuleni hapo, na mpaka tunakwenda mitamboni shule hiyo haina umeme
kwa sasa
Mmoja kati ya wanafunzi waliopigwa na radi hiyo
Manfred Mwageni anayesoma kidato cha kwanza shuleni hapo akielezea tukio hilo
amesema alishangaa kujikuta ametupwa chini na radi hiyo huku ikiwaunguza
wanafunzi wengine
Bofya play hapo chini umsikilize Mkuu wa Shule na majeruhi wakizungumzia tukio hilo kwa undani