Waliomdanganya Magufuli 'airport' kushughulikiwa


Rais Magufuli amefanya ukaguzi wa kushtukiza katika sehemu ya kukagulia mizigo na abiria ya uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere upande wa Terminal One ambako Mwezi Mei mwaka huu alitembelea kwa kushitukiza


Katika ukaguzi wa Mei, Rais Magufuli alibaini kuwa mashine za ukaguzi (Scanners) zilikuwa hazifanyi kazi.


Mara hii Rais Magufuli amebaini kuwa mashine hizo zinafanya kazi, baada ya kujionea yeye mwenyewe uhalisia wa namna mizigo inavyokaguliwa.


Hata hivyo amemuagiza Mkurugenzi wa uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Bw. Paul Rwegasha kuwachukulia hatua za kinidhamu maafisa wawili walitoa taarifa za uongo pindi alipofanya ukaguzi wa kushitukiza mara ya kwanza.


"Leo kweli mashine zinafanya kazi na mimi nimeona lakini wale walionidanganya mara ya kwanza nilipokuja, Mkurugenzi hakikisha unawachukulia hatua" amesisitiza Dkt. Magufuli.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo