Imebainika kuwa wafungwa wa Gereza la Kalilankulukulu
lililopo wilayani Tanganyika mkoani Katavi licha ya kukosa sare za wafungwa
Gerezani na kuwasababishia kukaa Utupu, wafungwa hao pia wanakabiliwa na
ukosefu wa maji safi na salama
Hali hiyo inawasababishia pia kutembea kwa miguu kwa
umbali mrefu wa kilometa 10 kuyatafuta maji
Hayo yamesemwa na mkuu wa gereza hilo Samwel Obete Lulu
wakati akitoa taarifa kwa mbunge wa viti maalum Mkoani Katavi Tasika Mbugo
pindi alipotembelea gereza hilo kwa ajili ya kuzungumza na wafungwa
Mbali na changamoto hiyo wafungwa hao hulazimika kulia
chakula mikononi badala ya vyombo maalum
Mbunge huyo amejitoa kwa kuwakabidhi shilingi 336,000/=
kwa ajili ya kununua vikombe, bakuli na sabuni za kuogea
Mkuu wa wilaya hiyo Salehe Mhando amemshukuru mbunge huyo
kwa moyo wake wa kujitolea huku akiiomba wizara ya mambo ya ndani ya nchi
kuliangalia suala la wafungwa wa gereza hilo na kulitatua kwani linakiuka haki
za binadamu