Waziri Ashuhudia Mateso wanayopata Viboko Kwa kupungua maji Katavi

Moja kati ya maeneo ya utalii ambayo Tanzania tumebahatika kuwa nayo ni pamoja na hii Mbuga ya Katavi ambayo utambulisho wake mkubwa ni nembo ya Viboko.

Lakini pia Viboko hao wengi wanaishi kwenye maisha magumu baada ya kuwepo kwa baadhi ya watu walioamua kuchepusha mto na kuharibu vyanzo vya maji, jambo ambalo limesababisha maji kutowafikia Viboko ambao maisha yao kwa asilimia kubwa yanategemea kuwepo kwa maji.

Na mmoja kati ya watu waliofika eneo hilo la Mto Katuma na kujionea ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, January Makamba ambaye yuko kwenye ziara ya kikazi kutembelea maeneo mengi nchini ili kujionea hali ya mazingira ilivyo.

Nimezipata pia Picha za Mbuga ya Katavi ambayo inatajwa kuwa na Viboko wengi lakini mazingira wanayoishi yamekuwa hatari kwako kutokana na kukosekana kwa maji ya kutosha.
cb9d6197-32e8-4669-8016-6df41f10e1a5
ecc12a10-43ff-44ac-9212-c7988f943792-1
dcfb3d25-b550-4aa9-ad66-58544595121a 96239c90-96f6-4ea6-9bec-fe5df653585a
4f1783b7-cb3b-40b7-b63e-5d0aa375b809


4acd1038-afad-4a2a-b5e0-b1284efb0c16

2ca5e1d2-8bf7-4e84-8d51-3af8abdf40c3
2c867457-d1f5-4304-a42e-253cf9a73d57


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo