Ujumbe wa Francis Cheka baada ya taarifa za kifo cha Thomas Mashali

Wiki hii imeanza kwa huzuni kwa mashabiki wa mchezo wa ngumi nchini baada ya kifo cha bondia Thomas Mashali hasa baada ya kusikia taarifa za chanzo cha kifo hicho. Mmoja wa watu walioumizwa na taarifa hizo ni Francis Cheka.
14719663_1520067368007074_7543799241525690368_n
Kupitia mtandao wa Instagram, Cheka ameandika:
Ilikuwa ni heshima kuingia ulingo mmoja na wewe ndugu yangu Thomas Mashari,
tulipanga tukutane tena 26/11, kweli hakuna aijuae kesho…
ila Mungu tu…
Ulale mahali pema peponi ndugu yangu, Mungu akutangulie…
We unatangulia si tunafuata,
Kila nafsi itaonja mauti…
Jina la Bwana lihimidiwe.
Wawili hao walikuwa ni wapinzani kwenye mchezo huo na wamefanikiwa kucheza mapambano kadhaa lakini Cheka amefanikiwa kuibuka mshindi kwenye mapambano mengi zaidi


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo